Viongozi wa kisiasa kutoka kwa serikali na upinzani wafariji familia ya mkuu wa majeshi Ogolla

  • | K24 Video
    86 views

    Viongozi wa kisiasa kutoka kwa serikali na upinzani, wameendelea kumiminika nyumbani kwake aliyekuwa mkuu wa majeshi Jenerali Francis Ogolla, kuifariji familia yake. Rais William Ruto, kinara wa azimio raila odinga pamoja na viongozi wengine, walifika kwa familia ya ogolla wakati tofauti. Wakati huohuo, muungano wa azimio unataka uchunguzi wa kina ufanywe, kubaini kilichosababisha kuanguka kwa ndege iliyomuua Jenerali Ogolla pamoja na maafisa wengine wanane waliokuwa pamoja naye hiyo jana.