Viongozi wa kisiasa na kidini wakashifu maandamano kaunti ya Kisii

  • | Citizen TV
    521 views

    Mwakilishi wa kike kaunti ya Kisii Dorice Donya Aburi kwa pamoja na baadhi ya viongozi wa makanisa kutoka kaunti hiyo wamekashifu misururu ya uharibifu unaoendelea kushuhudiwa wakati wa maandamano akisema kinachoshuhudiwa ni ubabe wa wanasiasa. Akizungumza maeneo ya Bomachoge katika hafla ya kutoa msaada kwa wasiojiweza katika jamii , Donya amesema kwamba japo gharama ya maisha imepanda viongozi wanapaswa kusitisha maandamano ya fujo ili kuzuia kupoteza maisha ya vijana nchini.