Viongozi wa makanisa wataka msasa wa mawaziri wateule kuzingatia maadili

  • | Citizen TV
    3,733 views

    Macho yote yanaelekezwa bunge la kitaifa pale watu 11 walioteuliwa kwenye baraza la mawaziri watakapopigwa msasa. Hata hivyo, viongozi wa kidini wanawataka wabunge kufanya uadilifu na makini wanapowapekua mawaziri hao wateule ili kuhakikisha wanaopitishwa ni wale watakaowaridhisha wakenya. Na kama Melita Ole Tenges anavyoarifu, Naibu Rais Rigathi Gachagua aliyeabudu kwenye kanisa eneo la Kayole ameendeleza wito kwa vijana kusitisha maandamano