- 4,036 viewsDuration: 3:11Viongozi wa Muungano wa upinzani wamekashifu vurugu za hapo jana zilizoshuhudiwa kwenye mkutano wao katika eneo la Kisii. Wanasiasa hawa wakijumuisha kinara wa DCP Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Naibu Kinara wa Jubilee Fred Matiangi na mwenzake wa DAP-K Eugine Wamalwa kwa kauli moja wamemshutumu waziri wa usalama Kipchumba Mukromen kwa kile wanasema ni kuagiza maafisa wa usalama kuvuruga mikutano yao. Wanasiasa hawa wamezungumza huku wakiendelea na mikutano yao maeneo ya Gusii kwa siku ya pili hii leo.