Viongozi wa Nyandarua wanataka hazina kujumuishwa

  • | Citizen TV
    118 views

    Hisia mseto zinazidi kutolewa kuhusiana na pendekezo la kujumuisha hazina za ufadhili wa karo ili wanafunzi wafaidi zaidi na kuafikia elimu ya bure nchini. baadhi ya viongozi hatika kaunti ya nyandarua pamoja na viongozi wa kidini wameitaka serikali kujumuisha basari zote wakisema kuwa kutolewa kwa basari kupitia hazina tofauti kunachangia utapeli na ubadhirifu wa pesa. baadhi ya hazina hizo ni basari ya rais, NG-CDF, NGAAF na basari zinazotolewa na magavana wa serikali za kaunti.