Viongozi wa ODM waitaka serikali ibdilishe mfumo wake wa ushuru

  • | K24 Video
    53 views

    Viongozi wa chama cha ODM akiwemo kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga wameikashifu serikali ya Kenya Kwanza kwa kuwaekea wakenya mzigo wa ushuru wa juu unaozidi kuwakandamiza . Akizungumza katika ibada ya kanisa mjini Kisumu, Odinga aliwataka viongozi wa kanisa la kianglikana kuwaiga watangulizi wao na kupaza sauti dhidi ya ukandamizwaji wa serikali kwa wakenya. Haya yanajiri huku viongozi mbali mbali wakizidi kuishinikiza serikali ya Kenya Kwanza kupunguza ushuru, ambao umesababisha gharama ya maisha kuongezeka.