- 137 viewsDuration: 2:00Viongozi kutoka pwani wameitaka serikali kutatua tatizo la ardhi pwani ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara. Wakiongea katika hafla ya kutoa hatimiliki huko miritini waziri wa madini na uchumi wa maziwa na bahari Ali Hassan Joho, Gavana wa mombasa Abdulswamad Sharif pamoja na viongozi wengine wametaka kukoma kwa ubomoaji wa makazi kutokana na utata wa ardhi. Uvamizi wa mashamba na walaghai wanaojidai kuwa ni maskwota umetajwa kama changamoto inayokumba wizara ya ardhi.