Viongozi wa serikali waapa kuendelea na michango ya pesa

  • | Citizen TV
    286 views

    Viongozi wanaoegemea serikali wameapa kuendelea na michango wanayosambaza kwa makundi mbali mbali, wakisema inawiana na sera na manifesto ya kenya kwanza. Wakizungumza katika hafla mbali mbali Jumamosi, viongozi hao walisema michango hiyo haimaanishi kuwa serikali haitaendeleza miradi ya maendeleo, bali ni nyongeza tu ili kuimarisha maisha ya wakenya.