Viongozi wa upinzani wameshutumu mauaji ya vijana

  • | Citizen TV
    6,381 views

    Viongozi wa upinzani wameshutumu vikali mauaji ya waandamanaji siku ya saba saba wakiutaja kuwa ukiukaji mkubwa wa sheria. Viongozi hao sasa wamewataka wakenya kusimama kidete kutetea katiba na haki yao ya kuandamana. Aidha upinzani umezua maswali kuhusu mauaji yaliyotekelezwa na watu wasiojulikana waliokuwa wakitumia magari bila nambari za usajili katika maeneo ya ngong na Kiserian.