Viongozi wa vijana wa Kisii wataka waliotekwa nyara waachiliwe

  • | Citizen TV
    839 views

    Viongozi wa vijana kutoka kaunti ya Kisii ndio wa hivi punde kukashifu kukithiri kwa visa vya utekaji nyara nchini. vijana hao wamemtaka rais William Ruto kuchukua hatua ya kukomesha mara moja visa hivyo. Wakizungumza kule, Riana, Bonchari kaunti ya Kisii katika hafla ya kipute cha kufunga mwaka, kilicholeta pamoja vijana zaidi ya elfu tano, viongozi hao wametaka waliokamatwa wote kuachiliwa huru.