Viongozi wanaoegemea Serikali, wamemsuta kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, kwa matamshi

  • | Citizen TV
    1,919 views

    Viongozi wanaoegemea Serikali, wamemsuta kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, kwa matamshi ambayo ameendelea kutoa kwenye ziara yake marekani, wakiitaja kuwa kampeni ya kimakusudi kuligawanya taifa kwa misingi ya kabila. Viongozi hao waliokita kambi katika kaunti za Tharaka Nithi na Laikipia, wamewarai wakaazi wa eneo la kati kuendelea kuiunga serikali mkono kwa madhumuni ya kujihakikishia maendeleo zaidi.