VIONGOZI WAONYA DHIDI YA UCHOCHEZI WA KIKABILA

  • | K24 Video
    3,334 views

    Viongozi wakuu wa taifa wametoa onyo kali dhidi ya siasa za kikabila, wakihimiza Wakenya kudumisha amani na umoja. Naibu Rais Kithure Kindiki, akizungumza mjini Meru, alipigia debe mshikamano wa kitaifa. Naye Spika wa Bunge la Taifa, Moses Wetang’ula, akiwa Kisii, alimkemea vikali aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa madai ya kuendeleza siasa za ukanda.