Viongozi wataka wizara ya kilimo kutanganza bei ya mahindi

  • | Citizen TV
    431 views

    Viongozi wa maeneo yanayokuza mahindi wameitaka wizara ya kilimo kufungua maghala ya serikali na kutangaza bei ya mahindi ili wakulima waanze kuuza mahindi kabla ya mazao yao kuharibiwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Viongozi hao wanasema ruzuku ya mbolea kutoka kwa serikali imeboresha mavuno ila sasa wanahofia kuwa huenda wakulima wakapata hasara iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa kunua mahindi yao. Aidha wamepinga ununuzi wamahindikutoka mataifa ya nje kabla ya wakulima kuuza mahindi waliyovuna.