- 4,470 viewsDuration: 2:02Mbunge wa Matungulu Stephen Mutinda Mule amemtaka Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki kujiandaa kuondoka mamlakani mwaka ujao akisema mgombea wa Naibu Rais ajaye atatoka ODM. Mule anasema dalili za kuondolewa kwake kama naibu rais zimeanza kuonekana. Naye Seneta wa Embu Alexander Mundigi amepinga njama yoyote ya kumuondoa Kindiki mamlakani akisema kuwa Naibu huyo wa Rais bado ndiye chaguo la Rais kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.