Visa vipya 389 vya Covid-19 vyathibitishwa

  • | KBC Video
    Taifa hili leo lilinakili idadi kubwa zaidi ya watu waliothibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 kwa muda wa siku moja. Hii ni baada ya watu 389 kubainishwa kuwa na virusi hivyo na kufikisha jumla ya watu wanaogua ugonjwa huo humu nchini kuwa 7,577. Watu watano zaidi wameaga dunia ilhali watu 88 zaidi wamepata nafuu. Wizara ya afya imeeleza wasiwasi kwamba baadhi ya Wakenya bado wanapuuzilia mbali masharti ya kudhibiti msambao wa ugonjwa huo licha ya kuwa hali hiyo haijadhibitiwa.. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #KBCNewsHour #KBClive