Visa vya ukeketaji vimepungua maradufu eneo la Kuria

  • | Citizen TV
    258 views

    Eneo la Kuria limerekodi visa vya chini vya ukeketaji mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana. Ripoti kutoka kwa afisi ya naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Mabera inaashiria kuwa wasichana sita pekee ndio waliokeketwa mwaka Huu na wasichana 73 waliokolewa kutokana na ukeketaji huo. Kupungua kwa visa vya ukeketaji huko Kuria kumechangiwa na juhudi za hamasisho mara Kwa mara zilizowekwa na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali katika vita dhidi ya tabia hiyo iliyopitwa na wakati. Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali a MICONTRAP Benter Adhiambo ambaye alikuwa akizungumza wakati wa kampeni ya kupinga ukeketaji katika kaunti ndogo ya Ntimaru alisema kupunguzwa kwa visa vya ukeketaji katika eneo la Kuria ni ishara kwamba mikakati iliyowekwa na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali inazaa matunda.