Vita dhidi ya unyakuzi wa ardhi Nairobi

  • | K24 Video
    25 views

    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi inachunguza madai ya unyakuzi wa ardhi ya ekari 5.12 eneo la Karen jijini Nairobi inayosemekana kumilikiwa na serikali ya kaunti ya nairobi. Inadaiwa kuwa ardhi hiyo ilinyakuliwa na kampuni ya DAVJON group ambayo sasa inaitaka serikali ya kaunti iilipe fidia ya shilingi bilioni 1.28. Gavana wa kaunti ya Nairobi ameishtumu hatua hiyo huku akidokeza kuwa takriban vipande vya ardhi mia saba vimenyakuliwa.