Vita vya maneno na kizaazaa zimeshuhudiwa wakati wa hoja ya kumbabdua Gavana Mwangaza

  • | Citizen TV
    2,133 views

    Vita vya maneno na sarakasi zimeshuhudiwa, siku ya kwanza ya vikao vya umma kuhusu hoja ya kutaka kubanduliwa kwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza. Japo kuna wale waliomtetea Gavana Mwangaza, wengi waliozungumza kwenye kikao cha leo wameunga mkono hoja hiyo. Kikao cha leo kilichoandaliwa katika ukumbi wa bunge la kaunti ya Meru kilizua mdahalo mkali, hali iliyolazimu vikao hivyo kusimamishwa mara kwa mara. Haya yanajiri huku kesi inayopinga shughuli ya kumbandua Gavana Mwngaza ikiwasilishwa mahakama kuu mjini Meru. Gavana Mwangaza kupitia wakili Elias Mutuma anasema kuwa, hoja iliyowasilishwa bunge la kaunti haikuzingatia sheria na haina uhaki.