Vita vya Ukraine: Putin asema Urusi inapigania ardhi yake ya asili nchini Ukraine

  • | BBC Swahili
    17,773 views
    Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema vikosi vya Urusi nchini Ukraine vinapigania mustakabali wa nchi yao ya asili, katika hotuba yake ya kila mwaka kuashiria ushindi dhidi ya Ujerumani ya Nazi katika Vita vya Pili vya Dunia. Licha ya uvumi angetoa tangazo kubwa hotuba yake ilijielekeza kwa kiasi kikubwa kutetea uvamizi wa Urusi. Aliunganisha vita vya Ukraine na ushindi mwaka 1945, akizilaumu nchi za Magharibi na Nato kwa kukataa matakwa ya usalama. #bbcswahili #Urusi #ukraine