Vita yapamba moto Ukanda wa Gaza

  • | VOA Swahili
    157 views
    Ukanda wa Gaza ulikumbwa na mapigano makali Jumatano huku mashirika ya misaada yakionya juu ya hatari ya njaa na mazungumzo mapya yakifanyika mjini Cairo ili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas na kuachiliwa huru kwa mateka. White House imemtuma mjumbe wake anayehusika na Mashariki ya Kati Brett McGurk kwa ajili ya mazungumzo mapya yanayohusisha wapatanishi na Hamas, siku moja baada ya azimio la Baraza la usalama la Umoja wa mataifa linalopendekeza sitisho la mapigano la mara moja kupingwa na Marekani. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.