Skip to main content
Skip to main content

Vuguvugu linalounga mkono upinzani huko pwani limempigia debe kinara wa wiper kalonzo Musyoka

  • | Citizen TV
    7,129 views
    Duration: 1:51
    Vuguvugu linalounga mkono upinzani huko pwani limempigia debe kinara wa wiper Kalonzo Musyoka kupeperusha bendera ya urais katika uchaguzi mkuu ujao. Wakiongea huko Mombasa Tononoka baada ya kikao cha faragha viongozi hao wamelalama kuwa rais William Ruto amekosa kutimiza ahadi kwa wapwani ikiwemo ajira, tatizo la ardhi na ugavi wa raslimali. Badala yake wanadai ufisadi umechangia wakenya wengi kukosa huduma muhimu.