Vyama vya UDA na ODM vyaweka mikakati ya kuandaa chaguzi za mashinani

  • | KBC Video
    20 views

    Chama cha United Democratic Alliance-UDA kimewahakikishia wawaniaji wa nyadhifa mbalimbali kwenye uchaguzi wake wa nyanjani kwamba shughuli hiyo itakuwa huru na wazi. Wakiongea wakati wa kikao cha uhamasisho kwa wawaniaji kutoka kaunti ya Nairobi, viongozi wa kitaifa wa chama hicho waliondolea mbali hofu kwamba viongozi ambao tayari wanahudumu wana nafasi bora ya kuchaguliwa wakati wa uchaguzi huo. Kwingineko chama cha Orange Democratic Movement, ODM, kimebuni kamati ya kitaifa ya ushirikishi yenye wanachama watatu ambayo itaongoza uchaguzi wake baadaye mwezi huu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News