Vyombo vya habari vyaetoa wasiwasi wa teknolojia ya akili unde kuchangia usambazaji taarifa za uongo

  • | KBC Video
    6 views

    Baadhi ya wadau wa vyombo vya habari wameelezea wasiwasi kwamba teknolojia ya akili unde itachangia usambazaji wa taarifa za uongo na kutatiza uadilifu wa tasnia ya uandishi wa habari. Wakati wa uzinduzi wa hati ya Whitepaper inayotoa suluhu kwa masuala muhimu katika sekta ya vyombo vya habari duniani, Mohamed Jalal ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shirika la habari la Emirates alielezea haja ya kuwapa wanahabari ujuzi hitajika kuwawezesha kutofautisha baina ya taarifa ghushi na uandishi wa habari halisi. Washirika katika mkutano huo walisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika mafunzo ya kidijitali na kutoa wito kwa wataalam wa vyombo vya habari kushirikiana na taasisi husika kuhakikisha uandishi wa habari unasalia kuwa nguzo ya kuenea ukweli na uwajibikaji katika enzi ya sasa ya kidijitali duniani.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive