- 182 viewsDuration: 2:08Vyuo vikuu vya umma nchini sasa vinakabiliwa na madeni ya zaidi ya bilioni 100 yanayotatiza shughuli zake. Katibu wa elimu ya juu Daktari Beatrice Inyangala ameiambia bunge kuwa madeni haya yamekaba koo taasisi hizi za elimu ya juu huku wabunge wakitaka majibu kuhusu ni kwa nini yanaendelea kupanda. Wakati huo huo, wabunge wametaka majibu kutoka kwa wizara kuhusu bajeti ya ziada ya shilingi bilioni 14.36 kuhakikisha shughuli za idara hiyo zinaendelea vyema