Waajiri wateta kuhusu kuongezeka kwa ushuru

  • | Citizen TV
    1,411 views

    Muungano wa waajiri nchini FKE umesema kuwa hali ya uchumi nchini inazidi kudorora kutokana na kuongezeka kwa ushuru kwenye mishahara ya wafanyikazi. Katika kikao cha kamati ya mazungumzo katika ukumbi wa Bomas, mkurugenzi mkuu wa FKE Jacquiline Mugo amesema sheria na mikakati ya kufufua uchumi ambayo serikali inatumia inazidi kuwa msumari moto kwenye kidonda.