Waandamanaji wataka majibu kuhusu aliyehusika na mauaji ya mwanaharakati Richard Otieno

  • | K24 Video
    3,726 views

    Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini kilichojiri baada ya mwanaharakati wa Molo Richard Otieno maarufu "Molo President ”kupatikana ameuwawa mita mia mbili kutoka kituo cha polisi. Wakazi waliojawa na gadhabu walivamia makafani ya elburgon na kuondoka na maiti, wakiandamana kukashifu mauaji hayo ambayo wanadai yamechochewa na siasa. Mbunge wa eneo hilo kuria kimani ametaka uchunguzi kamili kufanyika kubaini kilichojiri ila anakosoa hatua kuvamia makafani na kuchukuliwa kwwa mwili wa mwendazake kwani utatiza uchunguzi.