Waanzilishi wa Black Lives Matter : Tulipambana kubadilisha historia

  • | BBC Swahili
    Wanawake watatu ambao walianzisha vuguvugu la Black Lives Matter wameambia BBC wanaamini kuwa imebadilisha siasa. Garza na waanzilishi wenzake wa BLM, Patrisse Cullors na Opal Tometi, walizungumza kama sehemu ya simulizi ya wanawake 100 mwaka 2020 hafla ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao ya mahojiano makubwa na wageni tarehe 30 mwezi Novemba. Watatu hao walianzisha harakati za Black Lives Matter mnamo mwaka 2013 baada ya George Zimmerman kukutwa hana hatia baada ya kumpiga risasi kijana mweusi ambaye hakujihami,Trayvon Martin. #bbcswahili #ubaguziwarangi #wanawake