Waathirika wa dhuruma za kijinsia Kenya bado wanakabiliwa na ukosefu wa makazi salama

  • | VOA Swahili
    212 views
    Ukosefu wa makazi na vituo salama kwa wahanga wa dhuluma za kijinsia miongoni mwa wanawake na wasichana inasalia kuwa changamoto kubwa kwa waathirika. Japo hatua kadha zimepigwa hasa katika mitaa ya mabanda ambapo visa hivi hunakiliwa zaidi nchini kenya, mashirika ya kijamii yanayowanusuru waathiriwa wa dhulma za kinjisia wanahoji serikali imekuwa ikitoa ahadi tele bila ya kuangazia kwa kina kutafuta suluhu la kudumu la dhulma dhidi ya wanawake na watoto. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.