Waathiriwa Lamu hudhulumiwa na jamaa zao

  • | Citizen TV
    87 views

    Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu wanalalamikia idadi kubwa ya visa vya ubakaji na ulawiti vinavyotekelezwa na wanafamilia katika kaunti ya Lamu. Hii ni baada ya kubainika kuwa zaidi ya asilimia 70 ya kesi za dhulma ya kingono zinazowasilishwa katika mahakama ya Lamu zinahusisha wanafamilia ambao wanawadhulumu watoto walio na umri mdogo. na kama anavyoarifu Rahma Rashid visa vingi vimeripotiwa maeneo ya Mokowe, Hindi na Mkomani katika Kisiwa cha Amu.