- 91 viewsKundi la waathiriwa wa maandamano dhidi ya mswada wa fedha wa mwaka 2024 wametaka serikali kutoa pesa za fidia upesi kama alivyoahidi rais william ruto. Wakizungumza katika afisi za Amnesty International hapa jijini Nairobi, waathiriwa hao wanataka ufafanuzi kutoka kwa serikali kuhusu jopo la ushauri kuhusu mchakato wa kuwalipa fidia, wakisema kuwa hawajapata mawasiliano yoyote kuhusu fidia yao.