Waathiriwa wa mafuriko Mathare wapiga kambi shuleni

  • | Citizen TV
    268 views

    Huku idara ya utabiri wa hali ya anga ikisema kuwa mvua itaendelea kuongezeka hadi Jumapili katika baadhi ya kaunti, mamlaka ya barabara kuu imetoa tahadhari ya mafuriko katika baadhi ya barabara nchini ambayo inaathirika na maporomoko ya matobe na maji. Haya ni huku shughuli ya uokoaji ikiendelea katika mtaa wa mathare jijini nairobi. Zaidi ya familia 300 zilizoachwa bila makao katika eneo la Kiamaiko zinajisitiri katika shule ya msingi ya Valley Bridge. Makazi ya familia hizo yalisombwa na mafuriko usiku wa jumanne na kuathiri mamia ya wakazi.