Wabunge 30 kutoka chama cha Jubilee wakubali kushirikiana na rais William Ruto

  • | Citizen TV
    12,243 views

    Wabunge takriban 30 kutoka chama cha Jubilee wamekata kauli kushirikiana na rais William Ruto, wakisema haya baada ya kujumuika naye katika ikulu ya rais. Viongozi hao walisema ni wakati mwafaka kuweka kando tofauti za kisisasa na kushirikiana ili kufanikisha ahadi walizotoa kwa wakenya. Rais William Ruto akiwakaribisha aliomba ushiriakiano wao bungeni haswa wakati miswada inayolenga ajenda za serikali zitakapowasilishwa. Wabunge hao waliongozwa na mbunge wa Balambala Omar Shurie, mwenzake wa Eldas Adan Keynan na mwakilishi wa kike wa kaunti ya Isiolo Fatuma Dullo ambao walirai rais kuwasaidia kukabiliana na janga la baa la njaa.