Miaka kumi tangu ujio wa vituo vya kutoa huduma kwa pamoja mpakani Busia na Malaba (OSBP), wafanyibiashara mpakani Busia wamelirai bunge la Afrika Mashariki lenye makao Arusha Tanzania kuangazia upya sheria za kibiashara baina ya mataifa ya wanachama ili kuzing'oa sheria zisizo na manufaa kwa shughuli za kibiashara .
Wakizunguma kwenye mkutano uliowaleta pamoja wafanyabiashara mpakani Busia na wabunge wanachama wa kamati ya biashara na maswala ya jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye bunge la EALA, wamelalamikia kujikokota kwa kuanzishwa kwa ujenzi wa soko la Jumuiya mjini Busia ambalo usoroveya wake ulikamilika miaka mitano iliyopita.