Wabunge wa Meru kujiandaa kumng'atua Gavana Kawira Mwangaza

  • | KBC Video
    23 views

    Tofauti za kisiasa zimekuwa dhahiri katika bunge la kaunti ya Meru huku wabunge wa bunge la kaunti hiyo wakijiandaa kujadiliana kuhusu hoja tata inayolenga kumng'atua gavana Kawira Mwangaza mamlakani kwa mara ya pili chini ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuponea chupuchupu kung'atuliwa Disemba ya mwaka jana;;;;;;NATS;;;;Bunge la kaunti liliwashirikisha wananchi katika shughuli hiyo ili watoe maoni yao kuhusiana na hatima ya kiongozi huyo;;;;;NATS;;;;Jumatatu asubuhi wakazi walitoa maoni yao katika shughuli iliyotekelezwa katika kaunti ndogo tisa;;;;;NATS;;;;Shughuli hiyo iliungwa mkono na vilevile ikapingwa na wengine;;;;;UPS;;;Katika uwanja wa maonesho wa Meru, tofauti za wanamaoni ziliibua vita vya maneno;;;;;NATS (Residents fighting);;;;;;Hoja hiyo ya kumng'atua mamlakani iliwasilishwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo la kaunti Evans Mawira, aliyesema kuna makosa saba miongoni mwayo kutoshirikisha bunge hilo la kaunti kuhusu uteuzi wa maafisa, kuipa barabara jina la mumewe na kukosa kutii maagizo ya kufika mbele wa wabunge hao;;;;;;CUTS;;;;Wabunge hao wa kaunti watajadiliana kuhusu hoja ya kumng'atua mamlakani Jumatano wiki ijayo baada ya kukamilishwa kwa shughuli ya kuushirikisha umma kutoa maoni kwa mujibu wa sheria.

    KBC Channel 1 brings you the Mashujaa Day 2023 celebrations held in Kericho County. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive

    fight