Wabunge wa muungano wa Azimio watoa makataa ya saa 24 kwa IEBC kumrejesha kazini Ruth Kulundu

  • | K24 Video
    193 views

    Wabunge wa muungano wa Azimio wametoa makataa ya saa 24 kwa IEBC kumrejesha kazini naibu afisa mkuu mtendaji Ruthu Kulundu. Wabunge hao walifanya maandamano hadi katika makao makuu ya IEBC Nairobi jumba la Anniversary Towers wakimshinikiza Chebukati amrudishe kazini Ruth Kulundu baada ya kusimashishwa kazi kufuatia tuhuma za kushirikiana na makamishna wanne wa IEBC waliojitenga na mwenyekiti wa tume hiyo. Maandamano ya muungano huo yalizimwa na polisi kwa kutumia vitoa machozi na kulazimu wafuasi wao kutawanyika.