Wabunge watangaza msimamao baada ya kukosa pesa za hazina ya CDF

  • | K24 Video
    29 views

    Kikao cha bunge la taifa kiliisha leo ghafla baada ya wabunge wote kuondoka wakilalamikia kutopata fedha za ustawi wa maeneo bunge ,CDF. Wabunge hao wameapa kuwa shughuli zote za bunge zitakwama hadi pale watapopokea fedha hizo. Runinga ya K24 imebaini kuwa tangu mwaka huu wa kifedha uanze shilingi bilioni 22 kati ya 54 hazijatolewa na serikali kama ilivyoratibiwa na hali hiyo imelemaza shughuli katika maeneo bunge yote. Naibu spika Gladys Shollei alilazimika kuahirisha kikao kufuatia wabunge kufanya fujo.