Wadanganyifu wa mtihani wa KCSE kukabiliwa kibinafsi

  • | Citizen TV
    78 views

    Waziri wa elimu Julius Migos amesema kwamba waliopatikana na hatia ya udanganyifu kwenye mtihani wa KCSE unaoendelea watachukuliwa hatua kibinafsi na wala sio vyuo husika kwa jumla. Akihudhuria hafla ya uzinduzi wa mpangilio wa usimamizi wa vyuo vikuu wa mwaka 2025 hadi 2028, waziri Migos vile vile alisema kwamba wizara yake inaendelea kushirikiana na chama cha Wahadhiri nchini UASU, kwa lengo la kusitisha mgomo uanoendelea.