Maafisa wa afya na wadau wameimarisha kampeni kushinikiza matumizi ya mipira ya kondomu miongoni mwa vijana, kufuatia takwimu za kutisha zilizoonyesha kwamba asilimia 41 ya maambukizi mapya ya virusi vya HIV mwaka 2025 yalikuwa miongoni mwa vijana wa umri wa kati ya miaka 15 na 24. Wito huo ulitolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kondomu yaliyofanyika katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa na kuandaliwa na baraza la kitaifa la kudhibiti magonjwa ya kuambukiza-NSDCC, Wakfu wa huduma ya afya ya Ukimwi kwa pamoja na washirika wengine na kuwahusisha wanafunzi kutoka chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa, chuo anuwai cha pwani, chuo cha mafunzo ya baharini na asasi nyingine katika kaunti ya Mombasa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive