Wadau wa elimu Kajiado waibua mjadala mkubwa kuhusu hatma ya mtaala mpya wa CBC

  • | Citizen TV
    463 views

    Wadau wa Elimu wameibua mjadala Mkubwa kuhusu hatma ya Mtaala mpya wa CBC kwamba huenda kukawa na mkanganyiko wa kuendeleza mfumo huo wa Elimu baada ya wanafunzi wa gredi ya tisa kukamilisha masomo yao. Wanasema japo imesalia miaka miwili kabla ya wao kufika gredi hiyo, kufikia sasa hakuna mikakati kamili ya kuhakikisha wanafunzi wanachagua taaluma ambayo watasomea baada ya kukamilisha sekondari msingi.