Skip to main content
Skip to main content

Wadau wa elimu wasifia msaada wa elimu wa CDF kaunti ya Trans Nzoia

  • | Citizen TV
    83 views
    Duration: 1:58
    Maafisa wa elimu pamoja na wadau wa sekta ya elimu kaunti ya Trans Nzoia wamesifia hazina ya maendeleo ya maeneo bunge CDF wakisema imekuwa nguzo muhimu katika kuhakikisha wanafunzi kutoka familia maskini wanapata nafasi ya kuendelea na masomo. Wakizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa basari kwa wanafunzi katika eneo bunge la Kwanza, wadau hao wanadokeza kwamba, kupitia juhudi hizo, wanafunzi wengi wameweza kulipa karo na kurejea shuleni, jambo linalosaidia serikali kufanikisha mpango wa asilimia 100 wa uhamisho wa wanafunzi kutoka shule za msingi hadi sekondari. Hata hivyo, wadau hao wametoa wito kwa serikali na viongozi wengine kuimarisha zaidi hazina hiyo ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaidika.