Wadau wataka Kiswahili kifunzwe chekechea hadi chuo kikuu

  • | K24 Video
    32 views

    Wadau wa kiswahili wanaitaka serikali kupitia wizara ya elimu na taasisi ya ukuzaji mitaala nchini , KICD, kuweka msistizo wa kipekee katika kufanya kiswahili kuwa somo la lazima katika mfumo wa elimu nchini kuanzia shule za chekechea hadi vyuo vikuu. Wakizungumza katika mkutano uliondaliwa jijini Nairobi, wadau hao wamesema mfumo huo ni njia moja ya kuzingatia lugha ya kiswahili kama lugha ya taifa, lugha rasmi na lugha ya matumizi mapana.