Wafanyabiashara katika soko la Ahero watoa makataa ya siku saba kwa serikali kuimarisha usafi sokoni

  • | Citizen TV
    712 views

    Wafanyabiashara katika soko la Ahero kaunti ya Kisumu wametoa makataa ya siku saba kwa serikali ya kaunti ya Kisumu kuimarisha hali ya usafi katika soko hilo la sivyo wataandamana. Kulingana na wafanyabiashara hao, juhudi zao za kupata huduma za usafi kutoka kwa serikali ya kaunti zimeambulia patupu huku mikutano ya mara kwa mara ikikosa kuzaa matunda.