Wafanyabiashara wa vyuma vikuukuu katika kaunti ya Kakamega walaumiwa kwa wizi wa nyaya za umeme

  • | Citizen TV
    267 views

    Miezi michache baada ya serikali ya kitaifa kuondoa marufuku ya ununuzi na uuzaji wa vyuma vikuukuu nchini, sasa muungano wa wafanyabiashara katika sekta hiyo kaunti ya Kakamega umejitokeza na kujitenga na madai kuwa wanashirikiana na wezi wa nyaya na vifaa vingine vya umeme katika eneo hilo. Wakizungumza mjini Kakamega kwenye mkutano wa uhamasisho ulioshirikisha vitengo vya usalama, viongozi wa serikali kuu na wafanyabiashara wa vyuma vikuukuu, wameitaka serikali kutilia mkazo suala la kutoa leseni kwa wafanyabiashara halali. Aidha, wafanyabiashara hao wamewataka wananchi kuwa macho dhidi ya matapeli ambao wamejiingiza katika biashara hiyo kwa nia ya kuwaharibia jina