Wafanyakazi wa shirika la utangazaji nchini-KBC wana matumaini huku wasimamizi wakitangaza kuanzishwa kwa mifumo iliyoimarika kuhusu masuala ya wafanyakazi ambayo itabuni fursa zaidi kwa zitakazofanikisha wafanyakazi kupandishwa vyeo. Akizungumza alipoongoza hafla ya sherehe ya kufunga mwaka jijini Mombasa, Mkurugenzi mkuu wa shirika hili Agnes Kalekye pia alifichua mipango ya kuboresha studio za shirika hili huku wakiangazia upeperushaji wa vipindi zaidi vya kipwani, wanawake na vijana pamoja na ari mpya itakayohakikisha shirika hili linanakili faida.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News