Wafanyikazi wa mamlaka ya majani chai wamepigwa kalamu

  • | K24 Video
    198 views

    Wafanyikazi wanane wa mamlaka ya majani chai hapa nchini wamepigwa kalamu. Imesemekana wamekuwa wakishirikiana na uongozi uliong'atuliwa ambao unapanga njama za kurejea ofisini. Wakati huohuo wale ambao walitwaa uongozi katika kaunti ya Meru wameitaka serikali iwape usalama wa kutosha baada ya wasimamizi waliobanduliwa katika kaunti hiyo kufika katika afisi za viwanda tofauti za majani chai Alhamisi kwa lengo la kuchukua usukani.