Wafugaji wa ngombe wa maziwa eneo la Kabiyet, Nandi waandamana kulalamikia bei duni ya maziwa

  • | Citizen TV
    419 views

    Wafugaji wa ngombe wa maziwa eneo Kabiyet Kaunti ya Nandi ,wameandamana kulalamikia bei duni ya maziwa na vilevile usimamizi mbaya kwenye shirika wanalotumia kusambaza maziwa yao. Wakaazi hao wameandamana hadi afisi za shirika la Kabiyet dairies wakitaka majibu kuhusu kucheleweshwa na kupunguzwa kwa pesa za maziwa licha ya kufikisha maziwa yao kwa wakati ufaao.