- 132 viewsDuration: 2:06Wafugaji wa Ng'ombe kati kijiji cha Nkorienito huko Kilgoris wamehimizwa kujumuisha pato la maziwa kwa mashirika ya kilimo na mauzo nchini na ugenini ili kupata faida. Wakizungumza katika hafla maalum ambapo wakulima kutoka mashirika 300 katika eneo hilo walipewa vyeti baada ya mafunzo ya wiki moja, maafisa wakuu kutoka mamlaka ya biashara KNCCI wamehimiza haja ya wanasiasa kuwajibika kuimarisha pato la wafugaji.