Wafungwa waachwa njia panda baada ya Mbagathi kusitisha matibabu

  • | Citizen TV
    511 views

    WAFUNGWA WANAOTAFUTA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MBAGATHI SASA WAMEWACHWA NJIA PANDA BAADA YA HOSPITALI HIYO KUSITISHA HUDUMA ZAKE KWA IDARA YA MAGEREZA KWA MUDA WA MAJUMA MATATU SASA. HII NI KUTOKANA NA MALIMBIKIZI YA MAMILIONI YA MADENI AMBAYO HOSPITALI HIYO INADAI. KWENYE ILANI YAKE, HOSPITALI YA MBAGATHI IMESEMA HAKUNA HUDUMA ZA MATIBABU ZITAKAZOTOLEWA HADI DENI LOTE LITAKAPOLIPWA KIKAMILIFU