Waganda watawala mchezo wa pooltable kwenye shindano la Base Yetu

  • | Citizen TV
    774 views

    Mganda erick koech na marion kisakye ankah ndio washindi wa awamu ya nne ya michuano ya pool ya base yetu iliyoandaliwa Eldoret kaunti Ya Uasin Gishu. Koech aliyemaliza wa pili kwenye awamu ya tatu alimaliza utawala wa wakenya kwenye mashindano hayo akimlaza mkenya denis mwanga kwenye fainali iliyohudhuriwa na halaiki ya mashabiki. kwenye kitengo cha wanawake marion kisakye ankah alimzidi maarifa jackline muthoni. Waandalizi wa mashindano hayo ya base yetu wameitaka serikali kuwekeza kwenye mchezo wa pool kukuza vipaji.