- 235 viewsDuration: 2:32Waathiriwa wa ugonjwa saratani katika Kaunti ya Kwale wamelalamikia gharama ya juu ya matibabu wakisema baadhi ya vipimo havigharamiwi kwenye bima ya afya ya jamii SHA na kutaka serikali kuvijumuisha ili kuwapunguzia mzigo. Wakizungumza kwenye mkutano wa kila mwaka wa kundi la Keep Hope Alive waathiriwa hao wanasema fedha za kughramia saratani chini ya SHA hazitoshi na kwamba bima hiyo huisha kabla ya mwaka kukamilika. Aidha Wanaitaka serikali kuongeza wataalamu wa saratani na kuleta baadhi ya huduma karibu na wagonjwa ili kupunguza safari ndefu ya kutafuta matibabu.Keep Hope Alive ina wanachama 201, miongoni mwao ni wagonjwa 35 wanaoendelea na matibabu ya saratani